picture

WELCOME

Friday, January 21, 2011

ALIE JADILI NA KUWAPA RICHIMOND & DOWANS MKATABA WA KUFUA UMEME NINANI




MAGARI YA KIFAHARI NAYO HAYAKOSEKANI SEREKALINI
gari moja lina kadiriwa kuwa na thamani ya milioni 80 hadi milioni 280 !!!
 Jumla ya Sh. bilioni 75.2 zimelipwa na serikali kwa kampuni ya Richmond/ Dowans kama malipo ya kuweka mitambo nchini (capacity charge), kati Desemba, 2006 na sasa.

Kadhalika, kampuni hiyo imelipwa dola milioni 2.4 za Marekani (karibu sawa na... Sh. bilioni 2.5) kama fedha za kununua gesi inayoendesha mitambo hiyo.

Hayo yalielezwa jana jijini Dar es Salaam na Ofisa Mkuu wa masuala ya Fedha wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), Bw. Jamhuri Ngelime wakati wa mahojiano maalum na Nipashe ofisini kwake.
Alisema malipo hayo yanafanywa kwa ushirikiano wa Tanesco na serikali.

Alifafanua kuwa, shirika lake linalipia gharama za gesi inayofua umeme unaozalishwa na Dowans wakati serikali inalipia gharama za capacity charge.

Bw. Ngelime alisema jumla ya malipo yote kwa kampuni hiyo hadi sasa, ni dola milioni 63.9 za Kimarekani (karibu sawa na Sh. bilioni 77.7).                                                  

NASASA DOWANS KULIPWA BILIONI 94 BADALA YA bilioni 185 ??
Uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC Court), Novemba 15, mwaka huu..., chini ya Mwenyekiti Gerald Aksen na wasuluhihi Swithin Munyantwali, Jonathan Parker uliamuru TANESCO iilipe Dowans kiasi... hicho cha fidia.
“Jopo la wasuluhishi limeamuru zaidi ya sh bil. 36 (dola za Marekani 24,168,343) na riba ya asilimia 7.5 kwa mwaka inayofikia kiasi cha zaidi ya sh bil. 26 (dola za Marekani 19,995,626) tangu Juni 15, 2010 hadi fidia hiyo itakapolipwa,” imeeleza sehemu ya uamuzi huo.
Pia jopo hilo la wasuluhishi wa migogoro ya kibiashara liliamuru sh bil. 60 (sawa na dola za Kimarekani 39,935,765) na riba ya kiasi cha asilimia 7.5 ambayo ni sawa na sh bil. 55 (dola za Marekani 36,705,013.94) zilipwe kuanzia Juni 15, 2010 hadi wakati wa malipo.
Jopo hilo lilisisitiza kuwa ada na gharama za wasuluhishi na za utawala sh bil moja (dola za Marekani 750,000) kwa wasuluhishi wa ICC zinatakiwa zilipwe na pande zote husika.
“TANESCO wanatakiwa kumlipa mdai (mlalamikaji) sh bil. 3 (dola 1,708, 521), ikiwa ni gharama za uendeshaji wa kesi na gharama zingine na kwamba madai mengine yaliyotolewa na pande zote katika kesi hiyo yanatupwa.                
ATCL nao wanadaiwa-mwendo wa ufisadi kwakwenda mbele Hata hivyo, ATCL ina kitanzi kingine cha mkataba wa ndege ya kukodi aina ya Air Bus A320, iliyokodiwa mwaka 2007 kwa kampuni ya Wallis Trading Inc kwa mkataba wa mia...ka sita wakati ndege hiyo ni mbovu.
Taarifa ya serikali inaonyesha kwamba gharama za kuvunja mkataba huo ni dola za Marekani milioni 18.0.
Hadi Machi mwaka huu, ATCL ilikuwa inadaiwa dola za Marekani milioni 15.5 kutokana na malimbikizo ya gharama za kuikodisha Euro milioni 1.6 zitokanazo na matengenezo makubwa na Euro 104,000 kwa ajili ya malipo kwa kampuni iliyosimamia matengenezo ya ndege hiyo.
Kuhusu mazungumzo ya namna ya kulipa deni hilo, Waziri Nundu alisema bado hajapata taarifa za kina kuhusu yanayoendelea ATCL na kwamba akishapata taarifa atajua nini cha kufanya.
Kampuni ya ATCL imekuwa na matumizi makubwa ikilinganishwa na mapato ambapo taarifa ya serikali ya Aprili ilieleza kwamba kwa kipindi cha Julai mwaka jana hadi Machi mwaka huu, mapato yalikuwa ni sh bilioni 7.8 wakati matumizi yalikuwa ni sh bilioni 26 jambo lililosababisha hasara ya sh bilioni 18.

No comments:

Post a Comment