picture

WELCOME

Sunday, January 2, 2011

HUDUMA DUNI ZA AFYA TANZANIA

Hii ni hali katika hospitali zetu.Baadhi ya walipa kodi wakiwa wamelala au kukaa chini kutoka na uhaba wa vitanda na viti,sehemu ya pesa zao ndio zinatumika kujenga majengo ya kifahari.

Mwanzoni mwaka huu kama sio mwishoni mwa mwaka jana wat...u wengi walipiga kelele kuhusu kiasi cha pesa kilichotumika kujenga makazi ya gavana wa benki kuu.Baadhi yetu tuliamini serikali itaanza kujirekebisha kutoka na kosa hilo hasa baada ya kuwa waziri mkuu anayejulikana kama “mtoto wa mkulima” ambaye mara nyingi amekuwa akituashiria hapendi makuu.Sasa jumba la kifahari kama hili linajengwa on his watch, tutaanza kuona hata hiyo ya kukataa magari ya kifahari ni kujitafutia umaarufu wa kisiasa

No comments:

Post a Comment