Dk Ndalichako alisema kuna wanafunzi 42 kutoka baadhi ya shule walifanya mtihani wakati walikwisha ondolewa katika usajili baada ya kubainika kuwa sifa za kidato cha pili walizowasilisha hazikuwa sahihi. Alizitaja shule hizo na idadi ya wanafunzi kwenye mabano kuwa ni Ujenzi (4), Kahama Muslim (1) St John Seminari (1), Eckernforde (1), Seuta (1), Jamhuri (1) Mdanya New Vision (12) na Mseru (21). Dk Ndalichako alifahamisha kuwa watahiniwa 56 wa kujitegemea waliondolewa kwenye usajili kwa kutokuwa na sifa lakini walifanya mtihani huo. Alivitaja vituo walivyofanyia mtihani watahiniwa hao na idadi yao katika mabano kuwa ni Mwigo (29) na Twitange (27). Dk Ndalichako alisema mtihani huo ulifanywa na watahiniwa 177,021 na asilimia 50.40 ya watahiniwa wote, wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 69,996 sawa na asilimia 43.47 na wavulana ni 107,025 sawa na asilimia 56.28. “Mwaka 2009 watahiniwa waliofaulu walikuwa sawa na asilimia 72.51 ya watahiniwa waliofanya mtihani huo,” alisema Ndalichako
Alisema ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonyesha kuwa jumla ya watahiniwa 40,388 sawa na asilimia 11.50, wamefaulu katika madaraja I hadi III. “Wasichana waliofaulu katika madaraja I hadi III ni 12,583 sawa na asilimia 7.81 na wavulana ni 27,805 sawa na asilimia 14.62,”alisema Dk Ndalichako. Alisema idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani huo ni 46, 064 sawa na asilimia 52.09 ya waliofanya mtihani.
Alisema katika kundi hilo, wasichana waliofaulu ni 22,405 sawa na asilimia 48.41 na wavulana ni 23,659 sawa na asilimia 56.13. Mwaka 2009 watahiniwa wa kujitegemea 49,477 sawa na asilimia 54.12 walifaulu, alisema. Aliongeza kuwa watahiniwa 458,114 wakiwamo wasichana 216,084 sawa na asilimia 47.17 na wavulana 242,030 sawa na asilimia 52.83 ndio waliojisajili kufanya mtihani huo mwaka jana. “Mwaka 2009 watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 351,152, hivyo idadi ya watahiniwa imeongezeka kwa watahiniwa 106,962 sawa na asilimia 30.5,” alisema Dk Ndalichako na kuongeza:
“Waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2010 ni 441,426 sawa na asilimia 96.36 na watahiniwa 16,688 ambao ni sawa na asilimia 3.64 ya watahiniwa wote waliosajiliwa, hawakufanya mtihani. “Kuna ongezeko la watahiniwa wa shule 109,329 ambao ni sawa na asilimia 43.0 ikilinganishwa na idadi ya waliosajiliwa mwaka 2009. Watahiniwa waliofanya mtihani walikuwa 352,840 sawa na asilimia 97.04, watahiniwa 10,749 sawa na asilimia 2.96 hawakufanya mtihani,” alisema Dk Ndalichako.
Alifahamisha kuwa mwaka 2009 watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa walikuwa 96,892 na 2010 kulikuwa na watahiniwa 94,525 ikimaanisha kulikuwa na upungufu wa watahiniwa 2,367 sawa na asilimia 2.44 ikilinganishwa mwaka 2009. “Watahiniwa 88,586 wakiwemo wasichana 46,358 na wavulana 42,228 walifanya mtihani huo, watahiniwa wa kujitegemea 5,939 sawa na asilimia 6.28 hawakufanya mtihani.
Shule zenye watahiniwa zaidi ya 40 zilikuwa 3,194 na zenye watahiniwa chini ya 40 zilikuwa 489. Akizungumzia matokeo ya mtihani wa maarifa (QT), alisema watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 26,540 kati yao wasichana ni 16,101 na wavulana 10,439. Alisema mwaka 2009 jumla ya watahiniwa 25,040 walisajiliwa kufanya mtihani huo kukiwa na ongezeko la watahiniwa 1,500, sawa na asilimia 5.99 ikilinganishwa na mwaka 2009 na kwamba jumla ya watahiniwa 23,585, sawa na asilimia 88.87 ya
NJAA anaathiri watoto kusoma vizuri UMASIKINI unachangia elimu kudidimia..!!
DARASA LINAPO HAMIA CHINI YA MTI sijui kama wanaelewa vizuri wanachofundiswa.!!..
UALIMU NIWITO AU NIKAZI najiuliza ufaulu mdogo kwawanafunzi wadarasa la saba na sasa kidato cha nne..!!??..
MAJENGO MAZURI WALIMU WAPO WAKUTOSHA vifaa vya kufundishia je vipo vyoo nyumba za walimu ..!!??..
CHOO KINAPO KOSEKANA SHULENI shule bila choo ..!!??..
VIFAA VYA MAABARA kwajili ya utafiti vipo nakama vipi vinaendana na wakati je maabara zenyewe vipo katika shule ngapi tanzania..!!??
KATIKA HALI KAMA HII NYUMBA DUNI hapa niutambulisho waukosefu waelimu na umasikini ulio kithiri UMASIKINI WAKUPANDIKIZWA na elimu duni...!!??..
NAKOSA JIBU hapa ilikua enzi zaukoloni au nikarne hii ya 21 KWELI ELIMU NIUFUNGUO WA MAISHAlakini nielimu bora ndio itamkomboa mtanzania..!!!..
MIGOMO mashuleni na vyuoni chanzo nani na itadumu hadi lini je elimu nibora walimu wanapata stahiki zao ..!!..
JE uzuri wasare zashule na uzuri wamajengo ya shule huendana na ELIMU NZURI au elimu bora ..!!??.
UMAKINI AU uyakinifu wa mwanafunzi kuzingatia masomo humwezesha kufaulu vizuri maslahi kwamwalimu huchangia mwalimu kutoa elimu bora kwamwanafunzi
UMAKINI AU uyakinifu wa mwanafunzi kuzingatia masomo humwezesha kufaulu vizuri maslahi kwamwalimu huchangia mwalimu kutoa elimu bora kwamwanafunzi
shule zetu na elimu yetu italiwezesha taifa kutoka hapa tulipo ndani ya UJINGA UMASIKINI shule zetu na elimu yetu italiwezesha taifa kutoka hapa tulipo ndani ya UJINGA UMASIKINI MARADHI..!!?.MARADHI..!!?.
No comments:
Post a Comment