picture

WELCOME

Thursday, February 3, 2011

JE..!!.??. NIAHADI ZA MWANATANU ZILIZO SABABISHA WATANZANIA WA ENZI ZA MWALIMU WAWE WAZALENDO KIASI CHA KULITHAMINI TAIFA LAO NA TULITUMIKIA KWA MOYO WA DHATI ..

Ahadi za mwana tanu,na tanzania yetu ya sasa
...Chama cha TANU ni chama kilichosaidia sana katika harakati za kuikomboa nchi yetu katika makucha ya ukoloni chini ya Uongozi madhubuti wa Hayati Julius K. Nyerere.Malengo makubwa ya chama hiki ...ilikuwa ni ukombozi wa nchi yetu lengo ambalo kwa kiasi kikubwa lilitimia.Kinachonofurahisha sana ni jinsi viongozi wa TANU walivyokuwa na dhamira za kweli na kujitolea kwa hali na mali katika kuikomboa nchi yetu.
Lengo kubwa la post hii,ni kuwakumbusha wana... Facebook .. Ahadi za Mwana TANU,na kama bado ni relevant kwa wakati huu ambapo Tanganyika(Tanzania) imefikisha miaka 49 ya uhuru,zifuatazo ni ahadi za Mwana TANU enzi hizo;

1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja,
2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote;
3) Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umasikini,ujinga,magonjwa na dhuluma,
4) Rushwa ni adui wa haki.Sitapokea wala kutoa rushwa,
5) Cheo ni dhamana,sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu,
6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote,
7) Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu,na;

8) Nitasema kweli daima,fitina kwangu mwiko.
KWASASA TUNA AHADI ZIPI WATANZANIA NATUNATEKELEZA ZIPI ??

No comments:

Post a Comment