picture

WELCOME

Tuesday, January 4, 2011

UBUNIFU AU UMASKINI?

Ukipita katika mitaa mingi ya Dar es Salaam,Mwanza hivi sasa, utaona ‘version’ mpya ya antena za TV zikining’inia kwenye nyumba za watu. Hizi ni zile zilizotengenezwa kwa tubes za taa za umeme ambazo tayari zimekwishaharibika.

Kwa maelezo ya watu wawili watatu niliozungumza nao na ambao wamewahi kutumia ‘version’ hii ya antena wanasema kwamba zinaonyesha vizuri zaidi kuliko zile zilizokuwa manufactured kiwandani. Mimi sijazijaribu. Lakini watu hawa walionyesha kuwa siriaz katika maelezo yao. Hivyo, niko kwenye mwelekeo wa kuyaamini.

Hata hivyo, ‘version’ hii ya antena, ambayo kwa mujibu wa wale waliowahi kuitumia wanasema inauzwa bei poa sana, yaani robo ya bei ya zile zinazotengenezwa viwandani. Elfu 3 mpaka 5.

Swali ninalojiuliza, je, huu ni ubunifu ‘mpya’ au ni dalili za umaskini? Nawakaribisha wadau kujadili jambo hili. Mimi niko njia panda.

Swali jingine ni kuwa je, wanasayansi wetu pale Mlimani na kwingineko, wamejaribu kufanya utafiti juu ya ‘version’ hii ya antena? Wanasemaje juu ya ubora wake? Je, zinaweza kuwa na madhara yapi kwa watumiaji? Je, kuna namna ambayo zinaweza kuboreshwa ili tutengeneze kwa ajili ya ku-export na hivyo kuliingizia taifa mapato ya kigeni? Hapa unaweza kuongeza maswali yako mengine mengi.

No comments:

Post a Comment